Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ukerewe Ndugu Alfred Sungura amewataka makarani waongozaji wapiga kura,wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura kufanya kazi kwa uzalendo na weledi katika zoezi la uchaguzi mkuu utakaofanyika 29 Oktoba,2025 .
Ameyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya watendaji hao katika ukumbi wa Albino uliopo kata ya Bukongo huku akiwasihi kuboresha uwazi wakati wote wa zoezi.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa kushirikiana na mawakala wa vyama vya siasa vitakavyokuwepo vituoni huku akiwakumbusha kuwa msimamizi wa kituo ndiyo msemaji wa mwisho katika kituo cha kupigia kura.
Jumla washiriki 2524 wamepatiwa mafunzo ya siku 2 katika kuhakikisha zoezi la uchaguzi mkuu lifanyika kwa usahihi kwa kufuata kanuni,sheria na miongozo mbalimbali ya tume huru ya uchaguzi Tanzania.
Jimbo la Ukerewe lina jumla ya vituo 613 ambavyo vitatumika kwenye uchaguzi Mkuu huu katika kata 25 za jimbo hilo.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.