Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wiliaya ya Ukerewe ndugu Innocent G Maduhu ametoa maelekezo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba, 2019 katika kikao cha kwanza kilichofanyika katika ukumbi mkubwa wa mikutano katika halmashauri ya wilaya ya Ukerewe. Kikao hiko kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama siasa, viongozi wa dini, viongozi wa asasi za kiraia na wazee, kwa lengo la kupata maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019.
Akizungumza kwenye kikao hicho msimamizi wa uchaguzi ndugu Innocent Maduhu ametoa maelezo kuhusu maelekezo na matkwa ya uchaguzi wa Serikali za mitaa ambazo zipo kwenye kitabu cha KANUNI ZA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA NGAZI YA VIJIJI, VITONGIJI NA MITAA ZA MWAKA 2019. Baadhi ya maelekezo hayo ni pamoja na Tarehe rasmi ya kufanyika uchaguzi ambayo ni tarehe 24 Novemba 2019, vigezo vya wanachi wanao paswa kupiga na kupigiwa kura kushiriki kwenye uchaguzi na kipindi sahihi cha kundesha kampeni.
”Serikali za mitaa ndizo zinazounda Serikali kuu hivyo zapaswa kutiliwa maanani kiutendaji ili kupata maendeleo mazuri katika serikali za mitaa na serikali kuu kwa ujumla”. Alisema Maduhu akihimiza ushiriki wa dhati wa wananchi katika uchaguzi huo.
Akijibu baadhi ya maswali ya wadau walio hudhuria kikao hicho Maduhu amesema kila mwananchi atapaswa kupiga kura katika eneo alipojiandikisha kwa mujibu wa kanuni za uchuguzi wa serikali za mitaa. Pia amesema viongozi wa kiserikali wana nafasi sawa kama vile kutoa elimu, kumshauri msimamizi wa uchaguzi na hata kukemea pale inapopaswa.
Akihitimisha kikao hicho Maduhu amesema maswali mengi yaliyoulizwa majibu yake yapo kwenye KANUNI ZA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA NGAZI YA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA ZA MWAKA 2019. Pia amewahimiza wajumbe hao kutopotosha jamii bali wawe mstari wa mbele kutoa elimu na majibu sahihi kwa maswali watakayo ulizwa na wananchi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.