Wadau wa Sekta ya Uvuvi Katika kisiwa cha Ukerewe kwa pamoja wanekubaliana kuachana na Uvuvi Haramu kwani wameona hauna tija mambo hayo yamesemwa na wavuvi wenyewe katika kikao cha wadau wa Uvuvi pamoja na viongozi wa Wilaya kikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe Cornel Magembe ambaye alimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vicent Anney ambaye naye ni mdau wa sekta hiyo Katika eneo lake.
Wavuvi kutoka visiwa mbalimbali vya ukerewe wameeleza changamoto mbalimbali wakutanazo wawapo katika majukumu yao ikiwemo uhalifu ziwani, Uvuvi haramu na doria zinazoendelea.
Mhe Cornel Magembe Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe ameeleza kuwa pamoja na changamoto hizo Serikali anayoiongoza hapa Ukerewe itakomesha na kuhakikisha wavuvi wanamazingira rafiki ya kufanyia kazi.
Magembe amewataka wavuvi hao kuacha mara moja Uvuvi wa kutumia zana haramu. Ameongoza kikao katika maazimio kuwa wavuvi waanzishe umoja wao katika visiwa na wawe na mfumo mzuri wa mawasiliano ambao utaenda sanbamba na kuunda ushirika ili waweze kukopesheka.
“Wote waliotajwa kuwaonea wavuvi Uchunguzi utafanyika na wakithibitishwa basi hatua za kinidhamu zitachukuliwa”. Alisema Magembe.
Baada ya wadau kulalamikia ushuru wa Halmashauri Magembe ameelekeza pamoja na viongozi wengine kuwa vikao vya maamuzi vya Halmashauri vikao na kuona namna ya kuboresha ushuru huo ili hata wavuvi waliohama kurudi na kuongeza pato la Halmashauri na Nchi.
Mhe Vicent Anney Mkuu wa Wilaya ya Musoma amewapongeza wadau wotewaliofika Katika kikao hiko na amewasihi kuwa huo Ndio umoja unaohitajika kati ya viongozi na wavuvi pasiwepo na nafasi kati yao.
“Uvuvi Haramu mkiamua kuumaliza ninyi wavuvi mnaumaliza bila kutoa hongo kwa maafisa wa uvuvi”. Alisema Anney
Joseph Mkundi Mbunge wa Ukerewe(CCM) ameshauri Wizara kupitia Upya Sheria ya uvuvi na kuona namna mvuvi au mfanyabiashara wa samaki kisafirisha mazao yake bila kulipia ushuru kila mahali anapopita bali kulipa maramoja kule alipochukuli mzigo.
Alli Hamis Mambile Mwenyekiti wa CCM (W) amewataka wizara kuangalia namna maofisa wanaotekeleza doria mbalimbali ndani ya Wilaya iwe rafiki na sio onevu na pia ijikite zaidi Katika kutoa Elimu ya Uvuvi bora.
Mhe George Nyamaha Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Kagunguli (CCM) amewataka wavuvi kushirikiana kwani kupitia umoja wataweza kufanikisha mambo mengi ya msingi kwa manufaa yao na serikali.
“Lengo letu ni kuboresha uvuvi na kuwa na uvuvi wenye tija kwa mvuvi na kuongeza pato la Halmashauri na Serial”. Alisema Nyamaha.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.