Wadau wa uvuvi wilaya ya Ukerewe wamekutana kujadili changamoto zinazowakabili katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba sambamba na changamoto za mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha zinazowahudumia kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde,Christopher Ngubiagai amesema lengo ni kusikiliza, kuchambua na kusuluhisha changamoto za wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na kuhakikisha uwekezaji wao unaleta tija kwao na Wilaya kwa ujumla.
"...ni lazima tukubaliane kuwa uvuvi ndiyo kipaumbele chetu katika Wilaya ya Ukerewe hivyo lazima tuwekeze katika sekta hii, ni vema tubainishe changamoto tunazokumbana nazo ili tuangalie njia bora za za kuzitatua ili tuwekeze kwa faida..." Cde Ngubiagai.
Aidha Cde Ngubiagai amesema miongoni mwa changamoto zilizoainishwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vikundi vya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ni pamoja na vifaranga kuwa chini ya kiwango katika ubora na idadi inayoletwa, ucheleweshaji wa ugawaji wa chakula, tofauti kubwa ya idadi ya samaki wakati wa upandaji na uvunaji na mchakato wa maombi ya mkopo kutoka taasisi za fedha.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya ukerewe ambaye pia ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Wanchoke Chinchibera amewataka wafugaji hao kuboresha ulinzi na usalama kwa vizimba vyao, lakini pia kutoa taarifa mahala husika kwa changamoto iliyo juu ya uwezo wao kwa wakati.
Akitoa ufafanuzi juu ya changamoto zilizoelezwa Mzabuni wa usambazaji wa chakula na vifaranga kutoka katika kampuni ya Owners General Supply Antony Marwa amewaasa wavuvi hao kuwa na usimamizi mzuri na ufuatiliaji bora wa samaki wakati wa ufugaji, kuzingatia mazingira ya ufugaji lakini pia kupokea maarifa kutoka kwa wafugaji wakongwe na wataalam wa uvuvi ili kuepukana na changamoto zilizojitokeza.
Glacial Marugujo ni Afisa biashara wa Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) amesema mchakato wa utoaji mikopo ulichukua muda mrefu kwa sababu vikundi vingi havikukidhi maridhiano il
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.