Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estomihn Francis Chang’ah akiwa ameambatana na Meneja SIDO mkoa wa Mwanza Bw. Bakari Songwe na mratibu wa Uwezeshaji Wilaya Bw. Anord Mafuruu wamekutana na wajasiliamali wa kata ya Namagondo Wilayani Ukerewe ambao wanajishughulisha na ujasiliamali tofauti. Miongoni mwao wapo wanaojishughulisha na ushonaji wa nguo, ufundi wa pikipiki na mashine, na mafundi wa samani.
Mhe. Estomihn F. Chang’ah Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe amekabidhi vifaa vya ufundi (toolkit) 10 na cherehani 22 kwa wajasiliamali na vikundi katika kata ya Namagondo. Amewataka wote waliokabidhiwa vifaa hivyo kuvitunza na kuvitumia ipasavyo ili lengo la vifaa hivyo litimie. Amehimiza wananchi kufanya kazi kwa kuwezeshwa kukua kiuchumi kuwa sera ya nchi kwa sasa ni maendeleo kupitia uchumi wa viwanda, hivyo amewataka kuanza kujiunga katika vikundi iliwawezeshwe na kufanya kazi. “Uchumi wa nchi hauwezi kukua kama watu hawapotayari kufanya kazi” alisema Chang’ah.
Amewataka wananchi kutumia mafunzo waliyo yapata kuwasaidia kuweza kujua mbinu bora za mapato na matumizi ili iweze kuendeleza mtaji wake na kuweza kuongezeka kibiashara na kuachana na shughuli zinazowapatia kipato kwa njia ya udanganyifu, hivyo amehimiza ubunifu mkubwa ili kuweza kuinuka kiuchumi na amewataka kutokukata tama na kufanya kazi kwa bidii kama Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyosisitiza watu kufanya kazi kwa bidii.
Bw. Bakari Songwe ambaye ni meneja wa SIDO mkoa wa Mwanza ameeleza lengo kuu wa kugawa vifaa hivyo ni kuinua uchumi wa wananchi ha vijana ambao wanania ya kujishughulisha kwa bidii na kuweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vitakua na tija kwa mtu binafsi, jamii nan chi kwa ujumla. Akieleza Bw.Emmanuel Ngoinde Afisa Ufundi SIDO mkoa wa Mwanza ameeleza juu ya vifaa hivyo vilivyo gawiwa kwa wanavikundi na wajasiliamali wa kata ya Namagondo kuwa vimepatikana kupitia shirika lisilo la kiserikali la Tools For Self Reliance (TFSR) lenye makao yake makuu nchini Uingereza katika visiwa vya Wales ambao wakishirikiana na SIDO walianzisha kongano la mafundi walioko Namagondo (Village Clusters) kupitia dhana ya kongano vijana na watu wengi walipata mafunzo na walibainisha changamoto ya vifaa ambapo awamu ya kwanza walipewa vifaa vya ufundi uhunzi toolkit 14.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.