Wenyeviti wa vijiji 76, wenyeviti wa Vitongoji 513 pamoja na wajumbe wa Serikali ya Kijiji waapishwa rasmi kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe Cornel Magembe ameshuhudia viongozi hao wakilaviapo vyao vya uadilifu, utii na uaminifu mbele ya Mheshimiwa Hakimu Charles Bilomela.
Magembe amewapongeza viongozi wote waliopata nafasi ya kuongoza waitumie kuwatumikia wananchi na sio kwa maslahi yao binafsi Bali kwa maeneo watokayo pamoja na nchi kwa Ujumla.
Magembe amewataka kuwa viongozi wenye vielelezo kwani yeyote atakae enda kinyume na maadili hato sita kumuondoa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mhe George Nyamaha amewapongeza wote walioshiriki Uchaguzi na hasa waliopita kwa ushindi wa kishindo. Amewasisitiza kusimamia maadili na kishirikiana na watendaji wa Vijiji na kata katika kuwaletea wananchi maendeleo. ‘Suala la kusoma mapato na matumizi limekua changamoto nyie mkawasomee wananchi’ alisema Nyamaha akisisitiza uwazi na ushirikiano.
Nyamaha amewasisitiza washirikiane na wakusanya mapato walioko katika maeneo yao na wao kama viongozi wawekioo kwa kutoshiriki katika Uvuvi wa kutumia zana haramu.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ya Wilaya ya Ukerewe Ester A. Chaula amewaelekeza viongozi wote waliochaguliwa wafuate Sheria, kanuni na taratibu wakati wanatekeleza majukumu yao.
Aidha Msimamizi wa Uchaguzi Innocent G. Maduhu amewapongeza viongozi wote waliopata nafasi yakuongoza kuchukulia kazi hiyo kwa umakini. Nae Afisa Uchaguzi wa Wilaya Royald Matiko ameeleza kuwa zoezi limekamilika vizuri na viongozi wote baada ya kuapishwa wanaanza kutekeleza majukumu yao katika maeneo yao. ‘Chama cha Mapinduzi Ndio chama kilichopata ridhaa kwani kimepata viti vyote katika vijiji 76 na vitongoji 513’ alisema Matiko.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.