Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomihn Chang’ah amekabidhi Baiskeli 10 za miguu mitatu kwa walemavu wa kutotembea. Baiskeli hizo zimekabidhiwa katika eneo la hospitali ya wilaya Nansio ambapo wanufaika walikabidhiwa vyombo hivyo kwa matumizi ya kila siku.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe amepongeza kwa hatua nzuri iliyo fikiwa na hospitali ya wilaya Nansio kwa kuweza kutenga fedha na kuweza kuwawezesha wanafunzi kupata baiskeli zitakazo wawezesha kuhudhuria masomo yao shuleni na kuondokana na changamoto ya kufika shuleni na kupelekea walemavu kukosa elimu. Pia wajasiliamali walionufaika na baiskeli hizo zitawasaidia kuweza kufanya shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato binafsi na pato la taifa pia.Chang'ah amesisitiza kuwa juhudi ziwe endelevu walemavu wengi waweze kubainishwa ili wawekewe utaratibu wa kuwawezesha. pia amewaeleza kuwa ulemavu sio sababu ya kutokufanya kazi au kusoma hivyo baiskeli hizo ziwasaidie kufanya kazi na kusoma huku zikitunzwa vizuri.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya baiskeli hizo Mganga Mkuu wa Wilaya daktari Joshua Monge alisema baiskeli hizo 10 zimegarimu Tsh 5,090,000/- kutoka kwenye mfuko wa afya wa pamoja kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi na wajasiliamali walemavu katika shughuli zao za kila siku na kujiongezea kipato. Kata zilizonufaika ni pamoja na Irugwa, Bwisya, Bukiko, Ngoma, Murutunguru, Bukindo, Bukindo, Bukungu, Igalla, na Muriti.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.