Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde.Christopher Ngubiagai amewaasa walimu wakuu wa shule za sekondari na maafisa elimu kata wote kuwa wabunifu na wasikivu kwa kuzingatia kuwa sekta ya elimu ndiyo eneo pekee lenye uwezo wa kumjenga mtu awe bora au vinginevyo.
Akizungumza wakati wa kikao na walimu hao katika shule ya sekondari Bukongo Cde.Ngubiagai amesema uongozi mwema huanza kwa kusikiliza , kiongozi ambaye hasikii,hasikilizwi na kuwataka kuwasikiliza wanaowaongoza na kutoa maamuzi kwa hekima.
"..msikilize mwanafunzi,mzazi kwani usikivu huleta umoja,amani na uaminifu.."
Aidha amewataka walimu hao kuwa wabunifu kwa kuanzisha klabu za sayansi,TEHAMA sambamba na kuanzisha mifumo ya kuibua vipaji kupitia michezo na sanaa mbalimbali.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Vincent Augustino Mbua amewapongeza walimu hao huku akikiri kuwa pamoja changamoto mbalimbali za kijeografia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo walizonazo wameendelea kujitahidi kitaaluma na wamekuwa msaada mkubwa katika mazoezi mbalimbali ya kitaifa kama vile mitihani na uchaguzi.
".. mfanye kazi kwa kufuata miongozo,kanuni,taratibu na sheria zilizowekwa hasa sheria za manunuzi ili muepuke hoja zisizokuwa za
msingi.Mkumbuke suala la lishe ni agenda yetu ya kudumu."
Leonard Ngobolo na Pius Manda ni wakuu wa shule za sekondari Chabilungo na Mumbuga wao katika nyakati tofauti wametoa kongole kwa uongozi wa Ukerewe uliopo kwa kuchagiza mabadiliko na maendeleo ya kasi ndani ya Wilaya hiyo.
"..tunawaombea Mungu awalinde muendelee kuwepo,tunahitaji kuwa mfano mzuri wa kuigwa na Halmashauri zingine hapa mkoani Mwanza na taifa kwa ujumla.."
|
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.