Katibu tawala wa mkoa wa Mwanza ndugu Elkana Balandya amewaasa wananchi wa wilaya ya Ukerewe kujiandaa kushiriki uchaguzi mkuu utakaohusisha uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025 kwani ndio njia pekee ya kupata viongozi wanaowataka.
Amezungumza hayo katika maeneo tofauti wakati alipokuwa katika ziara ya siku moja akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza kwa ajili ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
".. kushiriki uchaguzi ni haki ya msingi ya kila mwananchi,muhamasishane mjitokeze kwa wingi mchague viongozi kwa maslahi yenu.."
Ndugu Balandya ametoa pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kwa kazi nzuri inayoendelea ya kufanya maboresho makubwa katika sekta ya elimu,afya, maji,miundo mbinu na barabara.
Aidha akiwa mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Ukerewe iliyopo kata ya Kagunguli ndugu Balandya amewataka wanafunzi katika shule hiyo kuwa mstari wa mbele katika masuala ya kupinga rushwa kwani ni adui wa haki na kuachana kabisa na matumizi ya dawa za kulevya ambazo ni hatari kwa afya zao.
Rahma Kagembe ni dada mkuu katika shule hiyo yeye amesema wanaelewa kuhusu rushwa na wajibu wao mkubwa ni kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Vincent Augustino Mbua amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa katika kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa viwango vya ubora vinavyotakiwa .
Miradi mingine iliyotembelewa ni kituo cha afya Kigara kwa fedha kutoka serikali kuu, ujenzi wa hoteli na maduka ya biashara kwa fedha za mapato ya ndani sambamba na barabara ya Sungura.
|
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.