Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Dkt Raphael Mhana pamoja na timu ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko Wilayani Ukerewe wamefanya mafunzo ya namna ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona. Mafunzo hayo yamefanywa Katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, madiwani, timu ya menejimenti ya Halmashauri, watumishi wa Halmashauri, watendaji wa Kata na viongozi wa dini.
Dkt. Mhana ameeleza kuwa Idara ya Afya imejipanga kukabiliana na ungonjwa huu na sasa kinachofanyika ni utoaji wa Elimu wa namna ya kujikinga kupata ugonjwa wa Corona, ametaja Kituo cha Afya Bwisya na Nakatunguru vimetengwa maalumu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa endapo wakiwepo Wilayani Ukerewe.
Dkt. Mhana ameeleza kuwa kila mmoja kwa sehemu yake achukue tahadhari za msingi ikiwemo kuacha kushikana mikono, kukumbatiana, kunawa mikono kwa sabuni kwa maji yanatotiririka.
“Joto kali kupita kiasi, Homa, mafua Makali, kukohoa, kuumwa kichwa, kubanwa mbavu, vidonda kooni na mwili kuchoka ni dalili za virusi vya Corona.’ Alisema Dkt. Mhana.
Aidha Dkt Mhana Ameeleza kuwa mtu ukiona dalili hizo atoe taarifa kwa watoa tiba ili wafike kumuhudumia na kuweza kupata uangalizi wa karibu zaidi.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe Cornel Magembe amewataka wananchi kuchukua hatua na tahadhari kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya na kunawa mikono mara kwa mara.
“Lengo la kuwaita na kuwapa elimu hii ya kujihadhari na virusi hivi vya Corona ni kwamba nanyi pia mkatoe elimu hiyo katika maeneo yenu kama ambavyo leo mmepewa.” Alisema Magembe.
Magembe ameelekeza kuwa Hairuhusiwi kwenda magereza, Mikutano yote ya kisiasa kutofanyika, Harusi sherehe kama sio lazima sana ni vema isogezwe mbele. Amezitaka ofisi za umma na zisizo na umma kuweka maji ya kunawa na vitakasa mikono kwa ajili ya watumishi na zoezi hilo lifanyike katika nyumba za ibada yani makanisa na Misikiti.
Magembe Amewataka Wafanyabiashara wanaotumia mianya ya ugonjwa huu kujinufaisha kwa kupandisha bei za bidhaa kiholela kuacha mara moja.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.