Wanawake wa Wilaya ya Ukerewe wametakiwa kujituma na kujishughulisha ilikuweza kujikwamua kiuchumi na kueleta maendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi taifa amesema hayo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya katika kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani tarehe 08/03/2018 iliyoadhimishwa katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Wanawake wa Wilaya ya Ukerewe wakiongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Hellen Rocky.
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani katika Wilaya ya Ukerewe yamefana na kuadhimishwa kwa namna ya tofauti mwaka huu ambapo wanawake wengi walijitokeza kutoka katika kata zote na wakapatiwa mafunzo mbalimbali yatakayomwezesha mwanamke wa Ukerewe kujikwamua kiuchumi na kusaidia nchi kufika adhma ya Nchi ya Viwanda.
Baadhi ya mada zilizowasilishwa kwa wanawake ni pamoja na leseni za Biashara na Elimu ya kulipa kodi, kilimo cha kibiashara, ufugaji wa kuku kimkakati,Ushauri wa kisheria na elimu ya vikundi. Akihitimisha mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ambaye ndio kaimu Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri amewataka wanawake kutengeneza vikundi na kupata usajili ilikuwawezesha kupata Mikopo itakayowawezesha kutekeleza malengo ya lakini ametoa maelekezo kwa vikundi vilivyosajiliwa kuhakikisha wanatekeleza shughuli zilizoainishwa katika maandiko yao na sio vinginevyo.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Uongozi wa Wilaya wa Chama cha Wanawake Tanzania (CWT) na viongozi wa wanawake kutoka vyama vya siasa nao wamewataka wanawake kuwa na umoja na kuhakikisha kupitia umoja huo wanajikomboa kiuchumi.
Maadhimisho ya siku ya Wanawake Machi 8 imebebwa na Kauli mbiu “kuelekea uchumi wa Viwanda, tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini”
Wanawake Wawilaya pia wameadhimisha siku hiyo pia kwa kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ambapo walitembelea Wodi ya wazazi, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume na wodi ya watoto. Akieleza katika Utoaji wa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa siku ya maadhimisho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi. Hellen Rocky amesemawanawake wanawatia moyo na kuwafariji wagonjwa hao kwa kuwapa zawadi na kuwatakia uponyaji wa haraka na kurudi katika majukumu ya ujenzi wa taifa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.