Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura Jimbo la Ukerewe wamepatiwa mafunzo sambamba na kula kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama wa vyama vya siasa ikiwa ni sehemu ya hatua muhimu katika kutekeleza majukumu ya tume ya uchaguzi Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika 29 Oktoba,2025 .
Akifungua mafunzo hayo mwakilishi wa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ukerewe Ndugu Joseph Maginga amewaasa wasimamizi hao kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yanayotolewa na tume.
Aidha Maginga amewataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa kushirikiana na mawakala wa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria na kuepuka kuwa chanzo cha malalamiko kwa vyama vya siasa vitakavyokuwepo vituoni.
Alphaxide Silas ni msimamizi wa kituo cha Bukongo kwa niaba ya wasimamizi wenzake amesema mafunzo ni mazuri,yanaeleweka na wapo tayari kwa kazi ambayo wataifanya vizuri na kwa weledi .
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.