Ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wameanza mafunzo ya siku 3 yaliyofunguliwa leo Agosti 4, 2025 na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ukerewe Ndugu Alfred Sungura.
Mafunzo hayo yatakayokuwa yanatekelezwa na tume huru ya uchaguzi Tanzania yanahusisha washiriki 50 kutoka kata 25 za Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe na yanalenga kuwawezesha kutelekeza ipasavyo kazi na majukumu ya tume .
Akihutubia hadhara hiyo ya wasimamizi ngazi ya kata Ndugu Sungura amewataka wasimamizi hao kusoma katiba ,sheria,kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na tume ya uchaguzi Tanzania ili zoezi lifanyike kwa ufanisi.
Aidha wasimamizi hao wamekula kiapo cha kujitoa kwenye vyama vya siasa sambamba na kuapa kutunza siri zoezi lililoendeshwa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe.Lucas Aminedavia Nyahenga.
Akihitimisha hotuba yake msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ukerewe Ndugu Sungura amewasisitiza washiriki hao kushirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya katiba, sheria, kanuni na maelekezo mbalimbali ya tume ya uchaguzi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.