Wataalam na watafiti wa ndani na nje ya Ukerewe wamekutana katika simpozia kujadili namna ya kuhifadhi na kutafiti lugha, fasihi na tamaduni za Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa halmashauti ya wilaya ya Ukerewe kwa lengo la kujadili mikakati madhubuti ya kulinda na kuendeleza tamaduni za Kikerewe.
Simpozia hiyo iliyoandaliwa na Waadhiri wa Chuo Kikuu cha Napoli L' Orientale (UNIOR) kutoka nchini Italia,Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Shirika la utafiti (ISMEO) na Shirika la Kuboresha Mienendo na Desturi kwa Ustawi (KUMIDEU) lililoshirikisha waadhiri wa vyuo vikuu, wanafunzi na wadau wa sekta ya utamaduni wamewasilisha mawazo tafiti mbalimbali kuhusu tamaduni za kikerewe hasa hasa lugha za asili.
Akiwasikisha mada ya lugha ya Kikerewe utafiti na changamoto Abel Lupalula kutoka SAUT amebainisha kutokuwepo kwa sera za lugha na kutokuwahusisha wazee wa mila ni chanzo cha kupotea kwa lugha ya asili.
Mwalimu Bartolomeo Mafuru yeye ameibua methali zaidi ya 600 za Kikerewe nakuthibitisha kuwa nyingi zimepuuzwa kwa kukosa urithi thabiti wa kizazi cha kisasa huku akiwaomba wazee wawarithishe vijana asili yao ili isipotee.
Simpozia hiyo imeonesha uwasilishwaji wa muziki wa Kikerewe kama Endeno, Endongo, Marimba na Enanga zilizowasilishwa na wazee wa Ukerewe ulioambatana na jumbe mbalimbali kwa vijana wa kisasa.
Mzee Sabato Chikore ni mpigaji wa muziki wa endongo yeye anashauri vijana wa sasa kuendelea kuheshimu miziki hiyo na kuirudisha kwenye hadhi yake ili kuenzi utamaduni wa Wakerewe.
Nje na lugha ya Kikerewe Kiswahili pia kimewasilishwa vyema na Bi. Flavian Aiello wa UNIOR ambapo ameeleza kuhusu utafiti wake wa Historia ya kiswahili nchini Kongo akibainisha kuendelea kukua na kuenea kwa lugha ya kiswahili ambayo imekuwa lugha pendwa na msaada kwa watu wa Kongo.
|
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.