Wazazi na walezi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe wameaswa kuunga mkono masuala ya uchangiaji chakula shuleni ikiwa ni sehemu ya kuchochea ufaulu na kuleta mazingira rafiki kwa wanafunzi kupenda shule.
Akizungumza akiwa katika mkutano wa hadhara kata ya Bukindo wakati wa muendelezo wa ziara zake za kutembelea wananchi kusikiliza kero mbalimbali na kuzipatia utatuzi Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde Christopher E.Ngubiagai amesema ubora wa elimu unaendana na lishe bora.
Amewataka wananchi wote kuhamasika kutoa vyakula shuleni huku akimpongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa sera ya elimu bila malipo.
"..Rais wetu ameturahisishia maisha kwa sera yake ya elimu bila malipo,tujisikie vizuri na sisi kuwa sehemu ya kuunga mkono juhudi zake katika maboresho ya elimu walau kwa kuwapa chakula watoto wetu wanapokuwa shuleni.."
Regina Stanslaus ni mkazi wa kijiji cha Musozi kata ya Bukindo yeye ameunga mkono masuala ya utoaji chakula shuleni huku akisisitiza serikali kuongeza wigo wa ajira kwa watoto wao punde wanapohitimu masomo.
Kero zingine zilizoibuka ni pamoja na upungufu wa walimu na matundu ya vyoo mashuleni ambapo Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuyashughulikia .
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.