WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa ameongiza mazishi ya ndugu zetu waliofariki kwa ajari ya Kivuko cha MV Nyerere ambao idadi yao imefikia 224 huku akiwataka watanzania kuwa watulivu, kufuatia Serikali imeisha anza kuchukua hatua na tayari maafisa wote wakuu wanao husika na kivuko hicho tayari wameisha kamatwa.
Majaliwa alisema Serikali imeisha chukua hatua ya kuleta kivuko mbadala ambacho kitafanya huduma zake kama ilivyozoeleka katika gati la Bugorola na Ukara, ili kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku.
Aidha Majaliwa alisema taarifa zinasema kivuko hicho kilikuwa kimebeba mizigo mingi na abiria zaidi ya 260 ndio waliokuwemo ndani yake na Mungu amesaidia miili 219 imetambuliwa na ndugu zao,214 zimeishachukuliwa tayari kwa mazishi na tisa itazikwa katika makaburi ya pamoja ikiwa kati ya hao tisa watano ndugu zao waliruhusu kuzikwa na wenzao wanne ambao hawakupata ndugu.
"Rais Magufuli alitangaza siku nne za maombolezo ambazo zitaishia Septemba 24 mwaka huu na ametoa pole kwa wananchi waliofikwa namisiba hiyo na watanzania wote na niwashukuru wanachi wa Ukara kwa jitihada kubwa ya kuwaokoa watu 40 wakiwa hai na mimi nitakuwa hapa mpaka shughuli itakayo kamilika na zoezi la uopoaji linaendelea mpaka Serikali itakapo toa taarifa ya ufungaji wa kazi hii,"alisema Majaliwa.
Aidha Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea na juhudi za kuimalisha usafiri wa majini katika Bahari na Ziwa Victoria katika mialo 140, ikiwemo Bezi,Bukondo,Kayenze na Senga itawekewa Kivuko,huku akitoa wito kwa watanzania kushirikiana na ndugu wa Marehemu kwa kuwafariji zaidi nasio kuwajaza maneno mabaya ambayo yatavuruga amani.
Majaliwa alishuhudia uvutwaji wa kivuko hicho ambao unafanya na wataalamu kutoka Songoro Marine wakishilikiana na Tamesa kwa kutumia mtambo kutoka kampuni ya Nyanza Road.
Akitoa taarifa za uendeshaji wa maafa hayo mwenyekiti wa kamati hiyo waziri Isack Kamwelwe alisema kivuko hicho kilitengenezwa mwaka 2004 kiwa na uwezo wa kubeba abiria 101 tani 25 na Magari matatu, kilifanyiwa ukarabati mwaka 2013 na 2015 nailipofika Julai 2018 kilifungwa injini mbili na gia box zake hivyo hakikuwa na hitirafu yoyote.
"Mpaka sasa vifo vimefikia 224 nakati ya hiyo miili ya wanawake ni 125,wanaume ni 71 watoto wa kike ni 17 na wakiume ni 10 na miili minne ambayo haijatambuliwa tayari tumeisha ichukua DNA ili ndugu zao wakijitokeza waweze kufanyiwa uchunguzi kama vinasaba vyao vinaendana na marehemu hao.
Naye mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella alimweleza waziri mkuu Kasimu Majaliwa kuwa wananchi ndio wamefanya kazi kubwa ya uokoaji wa watu 40 ambao walikuwa hai na Serikali iliokoa mmoja ambaye ni fundi mkuu wa kivuko hicho hivyo imeonyesha wazi ndani ya jamii ya Ukara kunauwezo mkubwa wa kuokoa watu ndani ya maji.
Nao Mbunge wa Jimbo la Ukerewe Joseph Mkundi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ukerewe George Nyamaha walisema mambo yasiyo jitokeza yanauwezo wa kuyafanyia kazi na yasijirudie tena na faraja wanayoweza kuipata wananchi wa Ukara na wilaya hiyo kwa ujumla ni kupata chombo ambacho nitakuwa imara kitasaidia kitasaidia kuendana na mazingira.
"Sumatra yupo mmoja na hana chombo cha usafiri na Ukerewe ina visiwa 38,wananchi wamekuwa na hawafuari utaratibu hivyo kungekuwa na watu wa kusimamia kusingelijitokeza kwa tukio hili,ajari ndogo ndogo ni nyingi kutokana na wananchi kutumia mitumbwi lakini kungekuwepo na chombo kikubwa na kikatumika kama ulivyo elekeza mkuu wa mkoa wa Mwanza kivuko kifanye safari zake mara nne yani kutoka Bugorola mara mbili na Ukara mara mbili ingesaidia sana,"walisema Nyamaha na Mkundi.
Aidha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu ,Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na Walemavu Jenista Mhagama alisema bado kuna wajibu mkubwa wa kulejesha Hali na kuendelea kujihakikishia miili yote unapatikana na imezikwa,wizara kukilejesha kivuko ina watanzania na wana Ukara wote wanakuwa na utulivu wanaendelea kutekeleza.
"Mheshimiwa waziri agizo ulilolitoa la fedha zote zihakikishwe zi mewekwa katika akauti na tayari imeishafunguliwa katika Benk ya NMB tawi la Kenyatta iliyopo wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza na namba zake ni 31110057246 na kwa Tigo pesa ni 0677030000 ambayo kuituma italeta jina la RAS Mwanza,"alisema Mhagama.
Akizungumza kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi katibu wa hitikadi siasa na uenezi wa Chama hicho Hamflay Pole pole alisema Rais Magufuli ametuma timu kuja kuhakikisha inaahirikiana na wananchi katika kipindi hiki kigimu.
"Serikali ya CCM itaendelea kuhakikisha inasimamia Irani yake ikiwa ni kuboresha huduma za usafiri katika ziwa Victoria pamoja na usimamizi na uendeshaji wa vyombo vya majini na kuwachukulia hatua watendaji wote wazembe,"alisema Pole pole.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.