Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Joseph Magufuli amemwagiza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Aizack Kamwelwe, kuwa fedha zaidi ya shilingi milioni 400 ambazo ni rambi rambi ya ajali ya kivuko cha MV Nyerere kujenga vyumba vya vitatu vya wodi ya watoto,wanawake na wanaume katika kituo cha Afya Bwisya kilichoo kisiwani Ukara.
Katika rambi rambi hizo fedha zilizopatikana ni zaidi ya milioni 900 ikiwa katika ugawaji wa pesa kwa ndugu wa marehemu zilitumika milioni 266,huku zaidi ya milioni 200 zitatumika kuwagawia watu zaidi ya 500 walioshiliki kufanikisha shughuli hiyo ambapo kila mmoja atagawiwa shiringi laki nne.
Akizungumza kwa niaba ya Rais waziri Kamwele wakati akihitimisha shughuli ya ukopoaji wa mili ya marehemu pamoja na kukinasua kivuko alisema,Rais anawashukuiru watanzania wote katika kufanikisha kazi hiyo ambayo ilikuwa imeleta simazi kubwa ndani ya Taifa letu.
“Rais ametoa agizo la fedha zaidi ya milioni 400 zijenge wodi ya akina mama,watoto na wanaume zitakazobaki milioni 200 watapaiwa wale wote walioshiriki kufanikisha kazi hii,suala la uchangiaji litasitishwa leo Septemba 29 majira ya saa saba kamili mchana,”alisema Kamwelwe.
Aidha alisema katika kuwaenzi ndugu zetu utajengwa mnara wa kumbukumbu katika eneo la makaburi na matumizi madogo madogo ya chakula kwa ajili ya mapishi,a fedha zake zitatoka k katika akaunti ya rambi rambi ndio itafanya kazi hiyo.
Naye Meja Jenerali RichardMakanzo alisema wametumia shughuli hiyo katika kuigawa makundi Matatu,ikiwa kukufunga ili kisiendelee kuzama,hatua yapili ni kukifunga maboya ya kujaza upepo(Air bags),tatu kukivuta na kukileta nchi Kavu kikiwa salama.
“Sheria za Kijeshi zinasema huwezi ukamliza vita kisha ukaondoka maana huwa kunamajeruhi waliovujika mikono na miguu,ambao wanaweza wakajifunga na kuendeleza mashambulizi mbinu hiyo ndio tumeifanya hapa ya kuhakikisha Kivuko kimefika kikiwa salama,matengenezo yake hayata kuwa makubwa na tutahakikisha tunatoa mizigo yote iliyosalia ikwemo gari amabalo nalo tayali lipo nchi kavu,”alisema Makanzo kwa niaba ya CDF.
Aidha kazi ya kukinasua kivuko hicho cha MV NYERERE kilichozama Septemba 20 mwaka huu,katika ziwa Victoria haikuwa rahisi lakini kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Jeshi la wananchi wa Tanzania na vikosi mbali mbali vya Polisi,Zima moto,Jeshi la akiba kwa kushilikiana na wadau mblimbali iwezeza kufanikiwa kwa urahisi.
Kivuko hicho hivi sasa kimetia nanga katika fukwe za kisiwa cha Ukara wilayani UKEREWE kikisubiri kukarabatiwa ingawa wapo waliotarajia kazi hii ingechukua muda mrefu,lakini jitihada za serikali za kukinusuru kivuko cha MV Nyerere zimeonekana, utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa umefanyika kwa ufanisi mkubwa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.