Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndugu Vicent Mbua ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu kwa kuruhusu jumla ya shilingi milioni 45.8 kupitia mradi wa BOOST ambayo imefanya manunuzi ya zana mbalimbali maalum kwa watoto wa elimu ya awali na shule za msingi 71 ndani ya Wilaya ya Ukerewe.
".. Wanafunzi wetu watajifunza kwa vitendo na hii inakwenda kuleta mapinduzi katika sekta ya elimu kwa kuzingatia umuhimu wa elimu ya msingi katika safari ya elimu ya mwanafunzi , serikali inaendelea kufanya maboresho katika sekta ya elimu Ukerewe kwenye miundo mbinu ,zana za kufundishia kama hivi wajibu wenu ni kuhakikisha vitatumika ipasavyo.." Amesema Mkurugenzi Mbua alipokuwa akizungumza na walimu katika shule ya msingi Bukongo wakati wa hafla ya ugawaji wa zana za kufundishia
Akiainisha changamoto katika utekelezaji wa mradi huo Afisa elimu maalum wa Halmashauri hiyo ndugu Francis Matiko amesema baadhi ya vifaa haipatikani kwa urahisi hapa nchini.
".. Masuala ya kuharibuharibu vifaa na kwenda navyo nyumbani kwa matumizi binafsi sio sawa.." Amesema Kaimu Afisa elimu msingi Wilaya ya Ukerewe Bi.Bahati Mwaipasi.
Adrea Majani na Anastazia Mkoji ni wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Bukongo wao wanashukuru kwa vifaa hivyo huku wakiahidi kufanya vizuri kitaaluma.
Vifaa vilivyonunuliwa ni pamoja na matawi ya namba,miti ya saa,vibao,vitabu vya consonati na matunda na vifaa vingine vya steshonari.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.