Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde.Christopher Ngubiagai anaendelea na ziara zake za kawaida kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.Akiwa kata ya Ngoma;
Amekagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kata ya Ngoma awamu ya kwanza katika eneo la zahanati ya Hamkoko, serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 250 kuwezesha ujenzi huo lengo kuu likiwa kuboresha huduma za afya kwa kuipandisha hadhi zahanati hiyo kuwa kituo cha afya.
Mradi mwingine uliotembelewa ni ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa na matundu 12 ya vyoo ambapo serikali kupitia mradi wa BOOST imetoa kiasi cha shilingi milioni 221 kukamilisha mradi huo.
Amewataka wataalam na mafundi husika kufanya kazi kwa weledi na uadilifu katika kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati kwa viwango vya ubora vinavyokubalika .
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.