Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Joseph Magufuli jumanne tarehe 4 septemba atafanya ziara ya kikazi wilayani Ukerewe, ambapo atazindua miradi miwili ya maendeleo mradi wa maji Nebuye na mradi a chuocha ualimu Murutunguru.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alisema, Rais atashuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo kati ya wakandarasi na Wizara husika, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja wilayani Ukerewe.
Alisema, siku hiyo hiyo atazindua mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru wilayani Ukerewe na baadaye mradi wa maji katika kijiji cha Nebuye wilayani humo.
Aidha, mbali na hayo atapata fursa ya kuhutubia wananchi wa wilaya ya Ukerewe kupitia mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Ukuta Mmoja Nansio.
Hata hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kumlaki Rais na kumuunga mkono kwa kufanya kazi ili kukuza uchumi wa mtu binafsi, wilaya,mkoa na taifa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.