Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mwasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amesema zoezi la uopoaji wa miili ambayo itakua imenasa na kugeuza kivuko na kukitoa majini bado linaendelea likiongozwa na jeshi la wananchi kwa kishirikiana na majeshi mengine.
“Mpaka kufikia jana meli ilikua imelala kifudifudi na sasa kimelala ubavu na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiongoza zoezi hili” alisema Kamwelwe.Pia amewashukuru watanzania mbali mbali walioguswa na wanaoendelea kuombea shighuli zinazoendelea Ukara.
Aidha Zoezi la kupokea michango bado linaendelea ambapo wadau mbalimbali wanaendelea kujitokeza katika kichangia wananchi wa Ukara waliopatwa na Janga hili, miongoni mwa wadau walio wasilisha michango yao ni Baraza la maaskofu Jimbo la Dar es Salaam wameweka kwenye akaunti ya maafa kiasi cha shilingi Milioni 25. Na Benki ya KCB Tanzania Zuhura Muro nayo imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 125 pesa imeshawekwa kwenye akaunti tayari. Nao Benki ya Shirika la Posta limeweka Milioni 10.
Kwa siku ya leo imepokelewa Milioni 160, Hivyo mpaka saa sita mchana fedha zilizochangwa zinafanya jumla ya shilingi 557,020,000/-
Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amesema zoezi la kugeuza bado linaendelea vizuri na matumaini ya kugeuza kivuko ni mazuri mafundi na wataalamu wanaendelea kufunga Air Bags (maputo magumu yenye hewa) ili kisaidia kivuko kisimama. Na wakati zoezi hilo lilipokua linaendelea maiti moja ikapatikana. “Tunaendelea na kazi mpaka itakapo kamilika” Mabeyo.
Mtanzania mmoja anaitwa Abel Michael amewasilisha kiasi cha 100,000/- na mwenzake John Salia ametoa 200,000/-.
Katika hatua nyingine zoezi la kutambua miili linaendelea ambapo kuna familia moja iliyoweza kufika na kutambua ndugu yao aliyefariki miongoni mwa ile miili minne iliyokosa ndugu yao. Baada ya mahojiano ya masaa matano na ofisi za utambuzi wakaridhiwa kuwa yule aliyezikwa ni ndugu yao hivyo familia imeonyeshwa kaburi namba 8. Alisema Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara anaesimamia utambuzi wa miili katika kituo cha afya Bwisya katika kipindi hiki cha ajali.
Zoezi la Kulipa wafiwa na manusura wa ajali limeanza na fedha zinazotumika ni hii iliyochangwa na watanzani.
Michango inaendelea kutolewa wadau mbali mbali wanaendelea kutoa kama Kanisa la EAGT waliotoa shilingi Milioni 5. Uwanja wa Ndege KIA Milioni 5, ATCL Milioni 10, River oil milioni 2, Olympic Oil milioni 10,
Jumla mpaka sasa ya fedha zote ni 589,320,000
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.