Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi Mkuu iliyotangazwa na tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 50 (6) na kifungu cha 62 (6) vya sheria ya uchaguzi wa Rais , wabunge na madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 vikisomwa pamoja na kanuni ya 23 na 26 za kanuni za uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani za mwaka 2025 zinaelekeza kuwa kuanzia leo tarehe 14 Agosti 2025 hadi tarehe 27 Agosti 2025 ni muda wa utoaji fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani.
Msimamizi wa Jimbo la Ukerewe Ndugu Alfred Sungura ameanza zoezi la utoaji fomu za uteuzi wa wagombea ubunge ndani ya jimbo la Ukerewe leo tarehe 14 Agosti 2025 huku wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata wakianza kutoa fomu za uteuzi wa wagombea udiwani.
Vyama ambavyo tayari vimechukua fomu kwa ngazi ya jimbo ni Chama cha Sauti ya Umma (SAU) , National League for Democracy (NLD), Alliance for African Farmers Party (AAFP) na chama cha Democratic Party (DP).
" Kura yako,haki yako, jitokeze kupiga kura "
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.