Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe leo amehitimisha shughuli kubwa ya uokoaji katika kivuko cha Mv Nyerere. “Shughuli kubwa imesha kamilika sasa hivi tunapisha kamati iliyoundwa na Mhe. Rais inayoanza kazi ili iweze kufanya kazi yake.
Hadi Muda huu baada ya kutoa shilingi laki nne kama alivyoagiza Mhe. Rais iliyopo kwenye akaunti tuna milioni 725,625,598/-.Na ameelekeza kuwa fedha yote itumike kujenga majengo ya wodi tatu na samani zake ndani na kama fedha itaongezeka na kisalia itatumika kujenga kituo cha afya Bwisya na sio katika maeneo mengi. Amesema Kamwelwe.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ameelekezwa na Rais kutafuta njia rahisi ya kujenga majengo hayo bila kutumia gharama kubwa za wakandarasi Badala yake atumie SUMA JKT.
Aidha vitu vilivyokuwa kwenye kivuko wakati imepinduka vimetolewa ikiwemo gari aina ya kenta yenye namba za usajili T554DBA, pikipiki DFPA 2313, baiskeli moja na baadhi ya vifaa vya umeme vya kampuni ya JUMEME inayotoa huduma ya Umeme kisiwani Ukara.
“Hapa ndio tumefikia mwisho wa zoezi ndugu zangu Asanteni sana” Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.