MRADI WA MAJI SAFI NANSIO
HALI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KWA MWAKA 2016/2017
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe inatekeleza miradi mikubwa miwili ya maji ambayo ni mradi wa maji Vijijni (Mradi wa maji Kazilankanda) unayofadhiliwa na Benki ya Dunia na mradi wa maji Mjini Nansio unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB) chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi Mwanza (MWAUWASA) kama mwajiri.
MRADI WA MAJI MJINI NANSIO
Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria Awamu ya Pili (LVWATSAN-II) katika Mji wa Nansio Wilaya ya Ukerewe ulisainiwa tarehe 22.12.2014 kati ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza (MWAUWASA) na mkandarasi Angelique International Limited –Vishwa Infrustuctures and Services Private Limited wa New Delhi-India.
Mkandarasi huyo amefanya kazi kwa mkataba Na./MWAUWASA/LVWATSAN-II/EAC/ W/2014/002 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika Mji wa Nansio.kwa ghrama ya Tshs. 10,904,762,789.00 ( Bilioni kumi milioni mia tisa na nne laki saba sitini na mbili elfu mia saba na themanini na tisa tu). Utekelezaji wa Mradi umefikia asilimia 99 na Mkataba umekwisha tarehe 31.07.2016.
Baada ya kukamilika kwa mradi asilimia 70 ya wananchi wa Mji wa Nansio wanapata huduma ya maji safi na salama.
Mafanikio
Hadi sasa mradi umekamilisha miundombinu mikuu kama ifuatavyo;
-Ujenzi wa chanzo cha maji Nebuye
-Ujenzi wa kituo cha kutibu maji safi na salama Nebuye
-Ujenzi wa matanki mawili ya kuhifadhi majisafi eneo la Malegea (lita 3,000,000) na Nebuye lita 350,000
-Ulazaji wa bomba za maji kilomita 50.9 za vipenyo.
Changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi
Utekelezaji wa Mradi huu umekabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo mkandarasi anatakiwa kuziondoa au kukamilisha katika mradi kwa mujibu wa mkataba kama ifuatavyo:-
Mkandarasi amalizie kazi ya kulaza bomba za maji 1.09 katika eneo la Kakerege
Mkandarasi afunge ‘gate valve’ kwenye maeneo yote muhimu ya mradi pamoja na ‘Air Valve’ kama ilivyooneshwa kwenye ramani yakiwemo maeneo ya Bulamba,Nakatunguru,Kakerege, Nansio, Nantare na Nebuye ili kuondoa tatizo la kufumuka kwa bomba mara kwa mara kwenye viungio.
Mkandarasi anunue viungio vilivyobaki vya dira za maji 1,500 alizoleta kama ilivyo kwenye mkataba
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.