Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni tatu, milioni mia saba na sitini (Tshs. 3,760,000,000.00) kutoka IMF UVIKO 19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Mia moja, hamsini na tano (155) katika Shule za Sekondari Ishirini na sita, vyumba vya madarasa kumi na mbili (12) katika Shule za Msingi shikizi tatu (03) na bweni moja (01) kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu katika Shule ya msingi Nansio Wilaya ya Ukerewe.
Kwa upande wa ujenzi wa shule za msingi shikizi tatu (03) na bweni moja (01) jumla ya shilingi milioni mia tatu na ishirini tu (Tshs. 320,000,000.00) zimetumika kukamilisha ujenzi huo ambapo Shule ya Msingi Kulazu ilipokea fedha kiasi cha shilingi milioni themanini (Tshs. 80,000,000.00) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne kwa shule ya msingi shikizi Lyegoba, Shule ya Msingi Kaseni ilipokea kiasi cha shilingi milioni themanini (Tshs. 80,000,000.00) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne kwa shule ya msingi shikizi Lyamwenge na Shule ya Msingi Igalla ilipokea kiasi cha shilingi milioni themanini (Tshs. 80,000,000.00) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne kwa shule ya msingi shikizi Kabazilo na Shule ya Msingi Nansio ilipokea kiasi cha shilingi milioni themanini (Tshs. 80,000,000.00) kwa ajili ya ujenzi wa bweni la kulala watoto wenye mahitaji maalumu.
Kupitia fedha za Uviko 19 serikali ilielekeza kiasi cha milioni mia tatu na arobaini tu (Tshs. 340,000,000.00) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi (Three in one) katika kituo cha afya Kagunguri, mradi huo umetengewa kiasi cha shilingi milioni tusini tu (Tshs. 90,000,000.00) na ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitari ya Bwisya, ujenzi huo umetengewa kiasi cha shilingi milioni mia mbili na hamsini tu (Tshs. 250,000,000.00) kukamilika.
Serikali kupitia fedha za Uviko 19 ilielekeza kiasi cha shilingi bilioni tatu na milioni mia moja (Tshs. 3,100,000,000.00) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mia moja, hamsini na tano (155) kwa jumla ya shule za sekondari ishirini na sita ikiwemoꓽMIRADI YA UVIKO.pdf
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.